Poem0014: Chimera.

Like the morning dew to a leaf, He refreshed my soul. Like a balm to a sprain, he soothed my grief. Erect on my feeble back hinds I stood, Before he blew me of my feet and cause me drunk~stagger. I remembered my name this time, for he called it. No one had. Like the …

Continue reading Poem0014: Chimera.

SHAIRI 0004: KWA LAAZIZI

Huenda nikayumba, nikapoteza njia. Huenda nikanena maneno mazito, Yanayoudhi na kunuka fe! Huenda nikakutia majonzi. Huenda nik'acha unayosema y'ende na upepo. Huenda nikajawa na kiburi, Niweke mguu shingoni mwako, Na kukukanyagia chini. Huenda nikawa kiumbe kisichotamanika, Kinachochukiza kila mwana na binti ya Adamu.                         …

Continue reading SHAIRI 0004: KWA LAAZIZI

SHAIRI0003: UPWEKE

Niwie radhi laazizi, 'nambie ulipo, Ul'enda wapi lakini? Kaniacha naugua, Mtima 'ngu wadhoofika siku baada ya siku Ulitoa ahadi 'tarejea bali s'oni dalili. Tafakuri zangu ovyo ovyo zanibeba, Busu zako za asali, Na kumbatio la mama, Nywele za singa, zilizolala sawia mabegani, Na macho ya uchawi, yanayounata moyo wangu kwa nanga, Kwenye mandhari yal'otulia tuli, …

Continue reading SHAIRI0003: UPWEKE

SHAIRI0002: LAITI

Si huku, si huko - wapi sikuranda, nikayumba... Lipi sikutenda - kwa wingi  wa mashobo Na kichwa kigumu na sikio lisilosikia dawa Wala la mwadhini Mama kasema lipi? Mwalimu je? Sayari ya athi  ikanipeleka chuo Chuo kilichokosa mwelekeo - kikanipepesa na kunirusha ovyo. Na baba... Laiti angalikuwa hai, Angalinionyesha tariki, Angaliniambia ukweli, Ukweli ninaougundua kwa …

Continue reading SHAIRI0002: LAITI

SHAIRI 0001: NAMPENDA HUYO

Nazama! Ala! kumbe nazama! Zigo zito nibebao, Moyoni, ndani, ndani kabisa. Haijalishi, nitalibeba! Kutamani kwesha anza, Kama ni kupenda, sijui! Lakini afadhali. 'Nivutia, sura, umbo. Yateka moyo, maneno, maongezi, yapendeza, macho, macho. Huyo! Ai! Nani huyo? Hivi, kwa nini hivi hisi? Waniita mjinga? Eeeh! Ujinga ni kupenda huyo? Basi! Iwe hivyo! Nampenda! Sana! Lini ataja …

Continue reading SHAIRI 0001: NAMPENDA HUYO